Israel kusitisha msaada kwa Palestina

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waziri mku nchini Israel benjamini Netanyahu

Maafisa nchini Israel wanasema kuwa serikali hiyo itasimamisha fedha kwenda kwa utawala wa Palesina siku moja baada ya utawala huo kutuma ombi la kutaka kuwa mwanachama wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.

Maafisa ambao hawakutajwa walisema kuwa baraza la mawaziri nchini Israeli limeamua kuzuia kutolewa kwa dola milioni 125 ambazo hutumiwa kuendesha shughuli za serikali ya utawala wa Palestina.

Hatahivyo afisa kutoka utawala huo (Saeeb Erekat) ameitaja hatua hiyo ya Israeli kama adhabu iliyo kinyume na sheria.

Ikiwa utawala wa Palestina utafanikiwa kujiunga na mahakama ya ICC itasababisha Israeli kufikishwa mbele ya mahakama hiyo kutokana na uhalifu kwenye sehemu inazokalia.