Shambulio la bomu laua watano, Somalia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mashambulio yanayofanywa Somalia

Mlipuko mkubwa wa bomu la kutegwa ndani ya gari umetokea karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mogadishu nchini Somalia.

Msemaji wa serikali ya nchi hiyo, amesema watu wanne na mtu aliyejitoa mhanga katika shambulio hilo, wamekufa.

Inaaminika kuwa Jeshi la Somalia ndilo lililokuwa limelengwa katika shambulio hilo, ambalo linadaiwa kufanywa na mtandao wa Al shabaab.