Vigogo ligi kuu ya England watesa FA

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Heka heka katika lango la Hull wakati Arsenal ilipoibuka na ushindi wa 2-0

Mechi kadha zimechezwa kuwania kombe la FA kwa vilabu vya ligi kuu ya England na vile vya madaraja mengine.

Mabingwa watetezi Arsenal waliweza kuwacharaza Hull City 2-0 ambao wameshindwa kulipa kisasi baada ya kushindwa katika fainali za mwaka jana timu hizo zilipokutana. Magoli ya Arsenal yalifungwa na Per Mertesacker pamoja na Alexis Sanchez.

Haki miliki ya picha v
Image caption Wachezaji wa Chelsea wakipongezana baada ya ushindi 3-0 dhidi ya Watford

Mechi nyingine zilikuwa kati ya Chelsea na Watford, Chelsea ikiibuka na ushindi wa 3-0. Nayo Machester United ikiishindilia Yeovil 2-0. Kwa upande wake Manchester City nao waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Shef Wednesday.

Crystal Palace ilipata ushindi mnono dhidi ya Dover wa mabao 4-0, huku Stoke City ikiicharaza Wrexham magoli 3-1. Sunderland nayo ilivuna goli 1-0 dhidi ya Leeds.

Mechi kumi zimechezwa ambapo kwa ujumla vigogo wa soka England wameonekana kupata matokeo mazuri.