Maandamano makubwa yafanyika Ujerumani

Image caption Baadhi ya wananchi wa Ujerumani

Maandamano makubwa yamefanyika nchini Ujerumani kwa wanaopinga na kuunga mkono uislamu na wahamiaji.

Taa zinazimwa katika mitaa ya mji wa Cologne nchini Ujerumani kupinga maandamano hayo yaliyopangwa kupinga Uislam na wahamiaji, yakiwa ya kwanza kufanyika katika mji huo wa magharibi mwa Ujerumani.

Kanisa kuu la Cologne, na madaraja yote yanayovuka mto Rhine yatakuwa katika giza kwa kipindi chote cha maandamano.

Meya wa mji wa Cologne, J├╝rgen Roters amesema kitendo hicho ni msimamo dhidi ya kile alichokiita ubaguzi usio na mantiki, na kutuma ishara kwamba wale wote wanaopanga kushiriki katika maandamano hayo wanahitaji kufikiri tena.

Maandamano hayo yametokea wakati mmoja na yale yaliyofanyika katika miji mingine, na kufuatiwa na maandamano kama hayo katika mji wa Dresden, ambako yamevutia maelfu ya washiriki