Shahidi wa Ruto ICC auawa Kenya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Naibu Rais wa Kenya William Ruto anakabiliwa na tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu

Mwendesha Mkuu wa Mashtaka nchini Kenya ameamrisha kufanywan uchunguzi kufuatia mauaji ya shahidi mmoja kwenye kesi inayomkabili Naibu Rais William Ruto katika mahakama ya kimataifa ya ICC.

Meshack Yebei,ametajwa na Wakili wa Bw: Ruto kama shahidi muhImu sana katika kesi hiyo.Bwana Ruto ameshtakiwa kwa kosa la uhalifu dhidi ya binadamu na kutajwa kuwa mmoja wa washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya 2007/08.

Maiti ya shahidi huyo ilipatikana akiwa na majeraha mabaya maeneo ya Magharibi mwa nchi.

Yebei alipotea Disemba 28 na wiki moja baadaye maiti yake ikapatikana ikiwa imeanza kuoza kwenye mto mmoja.

Familia ya marehemu imeitaka serikali kufanya uchunguzi kubaini aliyemuua mwanamume huyo na pia ili kutuliza nyoyo za familia.

Inaarifiwa familia hio ilipiga ripoti kwa polisi pale ambapo mwanamume huyo alianza kusema kuwa maisha yake yamo hatarini mwaka mmoja uliopita kabla ya mwili wake kupatikana wiki jana.

Kulingana na ripoti ya uchungUzi wa kifo chake uliofanywa katika hospitali ya Eldoret, Bwana Meshack alifariki baada ya kupigwa na kifaa gutu kichwani. Alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata kichwani mwake.

Mwili wa Meshack ulipatikana Jumamosi mchana karibu na daraja la mto Yala.

Familia ya Meshack ilitambua mwili wake hospitalini Kapsabet,baada ya kupokea taarifa ya kupatikana kwa mwili wa mtu karibu na mto Yala.Mwili wake ulipatikana baada ya kusakwa kwa wiki moja.

Dadake Meshack alisema kuwa Meshack alimwambia maisha yake yamo hatarini baada ya kutofautiana na watu kadhaa kuhusu maswala ya kisiasa.

Mahakama ya ICC imethgibitisha mauaji ya shahidi huyo. Imejitetea kwa kusema kwamba mahakama hio ilipma hifadhi salama lakini akaamua kurejea nyumbani ambako aliuawa.