Mbakaji ataka kusaidiwa kufa

Haki miliki ya picha SPL
Image caption Ubelgiji inaruhusu wanatu wanaotaka kufariki kusaidia kufanya hivyo kwa kudungwa sindano ya sumu

Wizara ya sheria nchini Ubelgiji, imesema kuwa mwanamume aliyepatikana na hatia ya mauaji na ubakaji sasa hatasaidiwa katika azma yake ya kutaka kufariki kama alivyokuwa ameomba.

Katika taarifa ya wizara hio, waziri Koen Geens, alisema, anaheshimu ushauri wa madaktari wanaomtibu mtuhumiwa huyo aliyeiomba serikali kumsaidia katika kifo chake.

Frank Van den Bleeken,aliwasilisha ombi lake kwa serikali kwambe asaidiwe kufa kwa kudungwa sindano yenye sumu ili kumwepushia msongo wa mawazo anaokabiliwa nao.

Kwa miaka mingi, mtuhumiwa huyo, alisema kuwa alishindwa kabisa kubadili au kukomesha tabia yake ya ubakaji na kutokana na hilo haoni uwezekano wowote wa kuachiliwa.

Uamuzi wa kesi hio, ni wa kwanza kumhusu mfungwa tangu sheria inayoruhusu watu wanaotaka kufariki kusaidiwa kufanya hivyo kuanza kutumika miaka 12 iliyopita.