Mfungwa aomba kifo ili apumzike

Haki miliki ya picha PA
Image caption Frank van den Bleeken akiwaza

Wizara ya sheria nchini Ubelgiji imesitisha mpango wake wa kusitisha uhai wa mfungwa wa mauaji na ubakaji,ambaye aliomba kifo chake kiharakishwe .

Maamuzi hayo ya kusitisha kifo,yamekuja baada ya daktari aliyeteuliwa kumchoma sindano ya sumu mfungwa huyo kukataa kutekeleza ombi hilo.

Mfungwa Frank Van den Bleeken alichagua afe mwezi Septemba mwaka wa jana,na alitoa sababu za kutaka kifo chake kiharakishwe ,mosi kutaka kupumzika kutokana na msongo mkubwa uliokuwa unamkabili,pili akijenga hoja kwamba hana nafuu yoyote itakayomfanya achoropoke makosa yanayomkabili,na tatu kubwa kuliko yote, kwamba binafsi hawezi kuizuai hamu yake ya kufanya ngono inayomsukuma katika ubakaji.

Hii ni kesi ya kwanza tangu sheria hiyo mpya inayoruhusu utekelezaji wa mfungwa kuruhusiwa kufa endapo ataomba adungwe sindano hiyo ya sumu tangu ilipotambulishwa nchi Ubelgiji miaka kumi na miwili iliyopita.