Nigeria yathibitisha kutekwa kwa kambi

Haki miliki ya picha AP
Image caption wanajeshi wa Nigeria

Waziri wa Ulinzi wa Nigeria amethibitisha kuwa kambi yake moja ya kijeshi mpakani mwa Nigeria na Chad, imetwaliwa na wapiganaji wa kiislaamu.

Mkuu wa jeshi la angani Alex Badeh, amesema kuwa wanajeshi wa Nigeria ndio waliokuwa katika kambi hiyo ya kijeshi, inayotumika na wanajeshi wa mataifa mbalimbali.

Kambi hiyo iliyoko kando ya ziwa Chad ilishambuliwa siku ya Jumamosi na wapiganaji wa boko haram.