Je,wanaume wasalie eneo la kujifungulia?

Image caption Mwanamke anayejifungua huku mumewe akishuhudia

Huku ikiwa kutengeza mtoto ni swala la furaha baina ya mke na mume,kujifungua ni uchungu ambao huwachiwa mwanamke pekee. kulingana na vitabu vitukufu, uchungu unaohisiwa wakati mwanamke anapojifungua ni laana na adhabu kwa wanawake kutoka kwa mungu baada ya Hawa kumdanganya Adam kufanya dhambi na hivyo basi kumuasi.

Mbali na kukaa katika chumba cha kujifungua wanaume wengi hupendelea kwenda mbali ama hata kusafiri wanaposikia wake zao wanataka kujifungua.

Hadithi kwamnba wanaume hutafuta sababu za kwenda mbali ama hata kujitafutia visafari zimehadithiwa wakati wake zao wanapokaribia kujifungua.

Baadhi ya sababu zinazotolewa na wanaume wakati huo ni kwamba hawawezi kukaa ndani ya chumba cha kujifungulia kwa kuwa kitendo hicho ni cha uchungu mwingi na kinatisha.

Je, unadhani wanaume wanafaa kuwa na wake zao wakati wanapijifungua?