Mbwa aliyetelekezwa apata ofa ya makazi

Haki miliki ya picha SCOTTISH SPCA
Image caption Mbwa Kai apata ofa kedekede za makazi

Mbwa aliyetelekezwa nchini Scotland ajulikanaye kwa jina la Kai amepatiwa ofa tele za makazi mapya.

Mambo yanaonekana si mabaya kwa mbwa aliyetelekezwa kwenye stesheni ya Treni akiwa na sanduku lenye mahitaji yake.

Mbwa huyu alikutwa katika Stesheni akiwa amefungiwa kwenye reli siku ya ijumaa juma lililopita.

Lakini wasamaria waliomnasua katika eneo hilo wanasema wamekuwa wakipigiwa simu mara nyingi na watu wakitaka kumpa makazi mbwa huyo.

Wasamaria wema hao wanasema Kai yuko katika hali nzuri na ni rafiki hivyo wanaamini kuwa wamiliki wa mbwa huyo ambao bado wanatafutwa walishindwa kumhudumia.

Taasisi hiyo ya msaada wa wanyama inatoa wito kuwasiliana nao kupitia namba ya msaada 03000 999 999 ikiwa kuna mtu atakuwa na taarifa kuhusu wamiliki wa Kai.