Wapiganaji watekwa nyara, Syria

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mpiganaji wa kundi la Islamic State

Baadhi ya askari kutoka katika kikosi cha polisi, kilichoundwa na wapiganaji wa Islamic State, wametekwa nyara.

Taarifa kutoka Syria zinasema kikosi hicho chenye msimamo wa kidini hupiga doria katika maeneo yanayoshikiliwa na kundi hilo la wapiganaji wa IS.

Kwa mujibu wa Shirika la Haki za Binadamu la Uingereza lenye makazi yake nchini Syria askari polisi wengi wa kundi hilo walivamiwa na kutekwa katika mji wa mashariki wa al Mayadeen.

Hayo yametokea siku moja baada ya taarifa kwamba kiongozi msaidizi wa kikosi hicho katika eneo hilo ametekwa nyara, kuteswa na kunyongwa na wauaji wasiojulikana.