Whatsapp yavunja rekodi ya 'ujumbe'

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mtandao wa Whatsapp

Kila siku zaidi ujumbe billioni 30 wa mtandao wa WhatsApp hutumwa kulingana na takwimu mpya zilizotolewa na afisa mkuu wa mtandao huo Jan Koum.

Pia kuna watumiaji millioni 700 wanotumia mtandao huo mara kwa mara.

Koum anasema kuwa shirika hilo linafurahia idadi kubwa ya wateja ilionao.

Lakini idadi hiyo ni kubwa mno na hivyobasi kuwa vigumu kuelewa.