Mlipuko wa bomu wawaua 30 Yemen

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mlipuko wa bomu mjini Sanaa nchini Yemen umewaua watu 30

Mlipuko mmoja umetokea katika gari nje ya chuo cha mafunzo ya Polisi katika mji mkuu wa Yemen-Sanaa.

Walinda usalama wanasema kuwa watu 30 wameuawa na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa.

Duru zasema kuwa mlipuko huo ulisikika kote nchini humo.

Hiyo ni miongoni mwa misururu ya milipuko nchini Yemen katika majuma kadhaa yaliyopita.

Mingi ya milipuko hiyo imekuwa ikilenga wapiganaji wa Shia Houthi, ambao wamechukua udhibiti wa maeneo mengi ya mji mkuu Sanaa tangu Septemba.

Inadaiwa kuwa wanaolipua mabomu ni tawi la kundi kuu la wapiganaji wa Al Qaeda.