Misikiti kadhaa yashambuliwa Ufaransa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Miongoni mwa waliopoteza maisha katika shambulizi la Charlie Hebdo ni wanahabari 10

Maafisa wa Mahakama nchini Ufaransa wamesema kuwa misikiti kadhaa imeshambuliwa tangu baada ya tukio la kushambuliwa kwa wanahabari katika Ofisi za Charlie Hebdo.

Msikiti wa mjini Le Mans magahribi mwa Paris ulishambuliwa na guruneti.

Baadhi ya Waislamu wameeleza hofu yao kuhusu kushambuliwa kwa jamii ya kiislamu nchini Ufaransa.

Watu 12 waliuawa na Watu waliokuwa wamefunika nyuso zao wakiwa na silaha na kuvamia Ofisi ya Wanahabari hao siku ya jumatano.

Sababu ya shambulizi hilo inakisiwa kuwa ghadhabu ya jamii ya Waislamu wenye msimamo mkali baada ya jarida moja linalomilikiwa na kampuni hiyo kuchora kikaragosi kinachokejeli uislamu.