Uchaguzi wa Sri Lanka wafanyika leo

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Usalama umeimarishwa katika vituo vyote vya kupiga kura

Mamilioni ya Raia wa Sri Lanka wanapiga kura, uchaguzi ambao unampambanisha Rais wa nchi hiyo Mahinda Rajapaksa na Mshirika wake wa zamani.

Rajapaksa,ambaye alikua madarakani tangu mwaka 2005, aliitisha uchaguzi miaka miwili iliyopita huku wachambuzi wa mambo wakitabiri kuwa atashinda uchaguzi huo.

Lakini wapo wengi wamekuwa wakimuunga mkono mshindani wake aliyekuwa waziri wa afya Maithripala Sirisena.

Ulinzi umeimarishwa katika kila kituo cha kupiga kura sababu ya hofu kuwa uchaguzi hautakuwa huru na wa amani.

Rajapaksa alijipatia umaarufu baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka 2009 lakini sasa anadaiwa kuwa na upendeleo kwa marafiki zake akiwapa nafasi za uongozi.

Nduguze wanashikilia nyadhifa za juu nchini Sri lanka , na wakosoaji wanamshutumu kuliendesha taifa hilo kama Mradi wa familia.