Taharuki Ufaransa watu zaidi wakitekwa

Image caption Eneo ambalo washukiwa wa Charlie Hebdo wamezingirwa nchini Ufaransa

Huku maafisa wa polisi wakiwazingira washukiwa wawili wa ugaidi , kuna taarifa mpya kwamba Mwanamume tofauti aliyejihami kwa bunduki, amewateka nyara watu ndani ya duka mjini Paris

Washukiwa wanaozingirwa ni wale waliowaua watu 12 waliokuwa wakifanya kazi na jarida la vibonzo la Charlie Hebdo.

Taarifa za mwanamume huyu mwingine kuwateka nyara watu 5 ndio zimejiri sasa hivi.,

Idadi kubwa ya polisi iliingia katika eneo la Porte de Vincennes Mashariki mwa Paris,baada ya mwanamume huyo kuripotiwa kufyatua risasi huku akiwateka nyara watu wnegine 5.

Inaarifiwa mshukiwa huyu ni yule aliyemuua polisi mwanamke mjini humo Alhamisi.

Washukiwa wa shambulizi la Charlie Hebdo pia wamewashika mateka watu kadhaa ambao idadi yao haijajulikana.

Washukiwa hao wanaarifiwa kujificha ndani ya kituo cha kupiga chapa na inasemekana wamesema kuwa wako tayari kufa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi wakipiga doria katika eneo la dammartin-en-goele ambapo washukiwa wa Charlie Hebdo wanadaiwa kuzingirwa

Watu Twelve walipigwa risasi na kufariki huku wengine 11 wakijeruhiwa,katika shambulizi la kwanza dhidi ya ofisi za jarida la Charlie Hebdo, jarida ambalo huchapisha vibonzona lenye uhuru wa hata kukejeli dini ya watu.

Shambulizi hilo limewashangaza watu nchini Ufaransa na kote duniani.

Watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa katika eneo la Dammartin-en-Goele yapata kilomita 35 kutoka Paris,lakini maafisa wamekana ripoti ya mauaji yoyote.

Mpango huo unajiri karibia masaa 48 baada ya shambulizi hilo katika afisi za gazeti hilo ambapo watu 12 waliuawa kwa kupigwa risasi.

Washukiwa hao wanaodaiwa kujihami vilivyo baadaye waliutoroka mji wa Paris wakitumia gari.