Bei ya mafuta yashuka zaidi

Haki miliki ya picha ap
Image caption Bei ya mafuta

Bei ya mafuta yasiyosafishwa imeripotiwa kushuka zaidi.

Siku ya ijumaa mafuta yalikuwa yakiuzwa kwa chini ya dola 49 kwa pipa.

Bei ya mafuta katika masoko ya kimataifa kwa sasa yameshuka zaidi ya nusu tangu mwezi Juni.

Mwandishi wa masuala ya kiuchumi wa BBC anasema kuwa uzalishaji mkubwa wa mafuta nchini Marekani na hatua ya nchi za muungano wa kuzalisha mafuta OPEC kutotaka kupunguza uzalishaji wa mafuta vimechangia kushuka zaidi kwa bei hiyo.