Wanajeshi wakabiliana na B.Haram Nigeria

Image caption Wanajeshi wa Nigeria

Wanajeshi nchini Nigeria wamekuwa wakipigana na wanamgambo wa Boko Haramu kwenye mji ulio kaskazini mashariki mwa nchi wa Damaturu.

Walioshuhudia wamesema kuwa wanamgambo hao walivamia mji huo mkuu wa jimbo la Yobe usiku ulipoingia.

Milio ya risasi na milipuko mikubwa ilisikika.

Wanamgambo hao wa Boko Haram walivamia mji wa Damaturu mapema mwezi uliopita lakini walitimuliwa na jeshi la Nigeria.