Shujaa Muislamu katika shambulizi Paris

Supermarket iliyovamiwa na gaidi mjini Paris Haki miliki ya picha other

Mamia ya wanajeshi wanashika zamu mjini Paris baada ya siku tatu za ugaidi zilizouwa watu 17, huku taarifa zikitokeza kuhusu jinsi mfanyakazi Muislamu wa supermarket ya Wayahudi mjini Paris alivyowaficha wateja 15 pamoja na mtoto mchanga wa mwezi mmoja wakati duka hilo liliposhambuliwa na gaidi.

Aliwaficha wateja kwenye chumba cha barafu.

Lassana Bathily, kijana wa asili ya Mali, aliiambia televisheni ya Ufaransa kuwa aliwaongoza wateja waliokuwa wamebabaika, hadi chumba cha chini kwa chini.

Alizima mtambo wa barafu na kuwaomba wakae kimya na alirudi juu dukani.

Baada ya duka hilo kukombolewa na askari wa usalama, Lassana Bathily alisema wateja walimshukuru kwa kunusuru maisha yao.