ICC:Yebei alikuwa akiwahonga mashahidi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption ICC

Mtu aliyepatikana amefariki nchini Kenya na ambaye alikuwa akihusishwa na kesi ya naibu rais wa Kenya William alikuwa akitumiwa kuwahonga mashahidi,mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita Imesema ICC.

Upande wa mashtaka wa mahakama hiyo umesema kuwa haukuwa na mpango wa kumuita mtu huyo Meshack Yebei kama shahidi kutokana na hilo.

Mwili wa Yebei ulipatikana magharibi mwa kenya mapema mwezi huu.

Wakili wake amesema kuwa angekuwa shahidi wa William Ruto ambaye amekana mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu.

Bwana Ruto ameshtakiwa na ghasia zilizozuka baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Ni kiongozi wa wadhfa wa juu katika serikali kushtakiwa na mahakama hiyo tangu ufunguzi wake zaidi ya muongo moja uliopita.

Mahakama ya ICC iliondoa mashtaka kama hayo dhidi ya rais Uhuru Kenyatta mwezi uliopita ikidai kuwa upande wa mashtaka umekuwa kuwatisha mashahidi na kwamba wamebadilisha ushahidi wao.