Kilevi:Watu zaidi ya 50 wafa Msumbiji

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Mwanamke aliyetengeneza bia ni miongoni mwa waliopoteza maisha

Serikali nchini Msumbiji imetangaza siku tatu za maombolezo nchi nzima baada ya zaidi ya Watu 50 kupoteza maisha baada ya kunywa kilevi kinachoelezwa kuwa na sumu.

Watu hao walikunywa kilevi hicho wakiwa msibani.

Watu wengine kadhaa waliokunywa kinywaji hicho siku ya jumamosi walikimbizwa hospitalini.

Maafisa wanasema wanaamini kuwa kilevi hicho cha kienyeji kilichotengenezwa kwa mtama na mahindi kilikuwa na sumu ya nyongo ya mamba wakati waombolezaji walipokuwa makaburini.

Sampuli za damu za walioathirika na pombe hiyo pamoja na sampuli za bia zimepelekwa mji mkuu wa nchi hiyo, Maputo kwa ajili ya uchunguzi.

Mwanamke aliyetengeneza pombe hiyo sambamba na nduguze ni miongoni mwa waliopoteza maisha.uchunguzi kuhusu tukio hilo unafanyika.