Wanawake 2 wajitoa muhanga Nigeria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Sio mara ya kwanza kwa jimbo la Maiduguri kushambuliwa

Wanawake wawili wamejitoa muhanga kwa kujilipua na bomu mjini Potiskum kaskazini mashariki mwa Nigeria.takriban watu wanne wameuawa kwenye shambulio hilo na zaidi ya arobaini wamejeruhiwa.

Siku ya jumamosi mwanamke mmoja alijipua kwa bomu mjini Maiduguri kaskazini mwa Nigeria na kuua watu 19.Mashambulizi haya yamefanyika baada ya kutolewa ripoti kuwa mamia ya watu wameuawa wiki iliyopita katika mji uliokuwa ulioshikiliwa na wanamgambo wa Boko Haram katika jimbo la Borno.

shuhuda mjini Potiskum ameiambia BBC kuwa mabomu mawili yalilipuka ndani ya dakika moja yakipokezana. Mabomu hayo yalilipuka katika soko ambako watu walikuwa wakinunua Simu za mkononi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Vijana siku hizi wanalazimika kujihami ili kujilinda kutokana na mashambulizi yanayofanywa na kikundi cha Boko Haram

Bomu la pili lililipuka katika eneo ambalo watu walikuwa wamekusanyika kuwasaidia waathiriwa wa shambulio la awali la bomu.

Daktari aliyetembelea eneo la tukio amesema alishuhudia mabaki ya mikanda iliyokuwa imefungiwa mabomu kwenye miili ya wanawake hao wawili.amesema kwa umri wanaonekana kuwa na umri wa mwanzoni mwa miaka 20.

Kundi la Boko Haram limewatumia wanawake kujitoa muhanga hasa wenye umri mdogo, mfano siku ya jumamosi mjini Maiduguri msichana anayeelezwa kuwa na umri wa miaka kumi aliripotiwa kujilipua kwa bomu na kusababisha watu 19 kupoteza maisha.

Watu wanaoukimbia mji wa Baga wamesema kwa kipindi cha wiki moja iliyopita mamia ya Watu waliuawa na Wanamgambo wa Boko Haram wenye silaha.