Vijana waliokamatwa danguroni waachiwa Misri

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Vijana walioachiliwa

Mahakama nchini Misri, imewafutia mashitaka wanaume 26 waliokamatwa baada ya msako wa polisi katika jumba au danguro la wanaume na kjushitakiwa kwa kosa la kuchochea watu kutenda uovu.

Wanaume hao walikamatwa mwezi jana baada ya wanaume wengine 8 kufungwa jela kwa kosa la kuonekana kartika kanda ya video ambayo ilidaiwa kuonyesha ndoa ya wapenzi wa jinsia moja.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu, yamelaani serikali ya Misri, kwa ambavyo inawatendea wapenzi wa jinsia moja hasa kwa kuwafnayia uchunguzi katika sehemu zao za siri ili kubaini ikiwa ni wapenzi wa jinsia moaj au la.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wanume katika jumba lililosemekana kuwa jumba la maovu

Ingawa mapenzi ya jinsia moja hayajapigwa marufuku nchini Misri kwa wengi jambo hilo ni mwiko kwa jamii.

Familia za wale waliofutiwa mashitaka zilisherehekea sana mahakamani wakati jaji alipotangaza uamuzi wake.

Mwandishi wa Jarida la Daily Telegraph aliyeshuhudia kesi hizo, alisema kwamba kulingana na mwakaili, angalau mmoja wa wanaume hao alikuwa amebakwa wakati akiwa rumande.

Aliongeza kwamba washitakiwa walikuwa wamesimama kizimbani wakiwa wamefungwa mikono pamoja huku wakifunika nyuso zao.

Wakati wa kukamatwa kwao , viongozi wa mashitaka walisema kuwa mmiliki wa danguro hilo, alituhumiwa kwa kugeuza nyumba kuwa danguro au jumba na maovu.