Udini,chuki marufuku,Ufaransa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri wa sheria wa Ufaransa Christiane Taubira

Serikali ya Ufaransa imesema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watu watakaobainika kujihusisha na masuala ya ugaidi na vitendo vya kueneza chuki kwa misingi ya tofauti za kidini na itikadi.

Waziri wa sheria wa Ufaransa Christiane Taubira amesema kuwa maneno ya chuki,ama vitendo vyovyote vinavyohusiana na ubaguzi wa kidini ni lazima vipigwe vita.

Mamlaka za kisheria za Ufaransa zimearifu kuwa hadi sasa tayari kesi 54 zimekwisha funguliwa dhidi ya wanao toa maneno yanayoashiria ugaidi ikiwa ni wiki moja tangu kutokea shambulio la kigaidi la gazeti Charlie Hebdo.

Ripoti kuhusiana na wanaoshikiliwa na mkono wa sheria wa Ufaransa ,mchekeshaji Dieudonné,anakabiliwa na mashitaka kufuatia kubainika kuwaunga