Je Irina na Ronaldo wametengana?

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Christiano Ronaldo

Kuna fununu kuwa Cristiano Ronaldo ametengana rasmi na mlimbwende muonesha vivazi Irina Shayk aliyekuwa mpenzi wake, hili lina pata ithibati baada ya kuonekana Irina ameacha kumfuata Ronaldo katika ukurasa wa Twitter.

Fununu za kuachana kwao zilianza kuzagaa mapema wiki hii kwamba wawili hao wametengana kwa kisa cha Irina kushindwakuonekana kwenye tukio la kupokea tuzo za Ballon d'Or usiku wa jumatatu ambapo Ronaldo alikuwa mshindi wa jumla.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption hapo mwanzo mambo yalikuwa hivi

Irina amezoeleka kuonekana mstari wa mbele kila wakati na kikosi cha Real Madrid katika matukio yote na taarifa za hivi karibuni kwenye chombo cha habari cha Ki Hispania kinaeleza sababu za Irina kutoonekana katika tuzo hizo kuwa ni kutokana na mahusiano yao kufukia tamati .

Gazeti la masuala ya michezo la El Mundo Deportivo linaeleza kwamba suala la kuachana kwao ni kama limethibitishwa kutokana na Irina kuto mfuata Ronaldo kwenye mtandao wa Twitter kama ilivyozoeleka.