Isarel inatupeleleza: Hezbollah

Haki miliki ya picha AFP
Image caption wapiganaji wa kundi la Hebollah

Kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Kilebanoni la Hezbollah amethibitisha taarifa zinazodai kuwepo mmoja wa viongozi wa juu ndani ya kundi hilo anatuhumiwa kutumwa na Israel kuwapepeleza.

Shekh Sheikh Hassan Nasrallah amesema kiongozi huyo anayetuhumiwa tayari anashikiliwa na kundi hilo tangu abainike miezi mitano wakati akifanya kazi kwenye idara ya usalama ya kundi hilo la Hezbollah.

Kauli ya Shekh Nasrallah imekuja siku chache baada ya kutolewa taarifa kupitia vyombo vya habari vya Lebanon zinazodai kuwepoa kwa ofisa wa ngazi za juu wa Israel miongoni mwa wapiganaji haoa ambaye yupo kwa kazi maalum.

Hii si mara ya kwanza kwa kundi la wapiganaji wa Hezbollah kujikuta wakiwa na watu wanaowapeleleza miongoni mwao

Hata hivyo Hezbollah imewahi tena kumbaini mtu aliyekuwa akiwapeleleza,japo kuwa kwa sasa usaliti huo unawakumba wakiwa katika wakati mgumu wa mapigano dhidi ya serikali ya Rais Assad.