Walio na 'mipango ya kando' mashakani

Haki miliki ya picha SGL
Image caption Kifaa cha Semenspy

Waswahili husema kwamba siku za mwizi ni arobaini.Msemo huo sasa huenda ukafanikishwa miongoni mwa akina baba ambao huenda kinyume na ndoa zao na wabakaji.

Hii ni baada ya kubuniwa kwa kifaa kwa jina Semenspy kilicho na uwezo wa kubaini majimaji yaliosalia katika chupi,nguo za kulalia,katika nguo na maeneo mengine baada ya mtu kuhusika katika tendo la ngono.

Kulingana na gazeti la the Nairobian nchini kenya,kifaa hicho pia kina mwongozo unaofanya mambo kuwa rahisi kwa wanandoa walio na shauku miongoni mwao.

Maagizo yake ni kwamba iwapo unamshuku mumeo ama mkeo tafuta majimaji hayo katika chupi ama nguo zilizotajwa hapo awali.

Kama kifaa cha kupima iwapo mwanamke ni mja mzito Semenspy kinaweza kubaini mara moja iwapo mtu ana uhusiano mwengine nje.

Kulingana na daktari Wachira wa DIY Solutions,kifaa hicho kimetengezwa Marekani.Wachira amebaini kwamba amefanikiwa kupata majibu sahihi kutoka kwa wanawake wanaotaka kujua iwapo waume zao na marafiki zao wa kiume wanawadanganya katika uhusiano.

Si rahisi kuwakamata wapenzi wanaodanganya kwa kuwa kunahitaji upelelezi zaidi na subra.

kwa kuwa kuna maji maji ya mbegu za kiume katika chupi ya mwanamume sio ushahidi kwamba mwanamume huyo anakwenda nje ya ndoa.

Swali ni vile utakavyoonyesha ushahidi kwamba maji maji hayo yanatoka kwa mwanamume huyo kwa kuwa mara nyingi wengi hutoa maji hayo bila ya kuhusika katika tendo la ngono.

Daktari Wachira ana shauri kwamba mwanamke anayemchunguza mumewe anafaa kukaa kwa mda bila kufanya mapenzi, ili kuweza kuchukua sampuli za maji maji hayo kutoka kwa nguo za mumewe ama mpenziwe.

Anasema kuwa violezi hivyo vinafaa kuchukuliwa mara tatu na kutoka nguo tofauti za mpenzi anayeshukiwa.

Anasema kwamba si kila mara kwamba maji maji ya mbegu za kiume humtoka mwanamume bila ya kufanya mapenzi kwa hivyo hhiyo haifai kuwa sababu ya mwanamume kujilinda.