Algeria kuchuana na Afrika kusini

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wachezaji wa Afrika kusini wakikabiliana na wenzao wa Misri katika mechi ya dimba la mataifa ya Afrika 2011

Algeria yenye wachezaji nyota Yacine Brahimi, Sofiane Feghouli na Islam Sliman ambao umoja wao unatakiwa kufahamika kama utatu wa dhahabu wanataka kuanza kwa uimara michuano hii.

kutokana na uwepo wa wachezaji wenye kiwango cha juu watu wengi wanaipa Algeria nafasi kubwa ya kushinda michuano hiyo, lakini kocha Christian Gourcuff amepuuza mtizamo kuwa timu yake ina nafasi kubwa ya kutwaa kombe.

Afrika Kusini wao wanayatoa mashindano hayo kwa kumuenzi Senzo Meyiwa, aliekua nahodha wa timu ya Taifa ambaye aliuawa mwezi Oktoba mwaka jana.

Kocha wa kikosi cha Afrika kusini Ephraim "Shakes" Mashaba ameeleza kwa upande wake "hatuna sababu ya kuogopa wapinzani wetu.".

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wachezaji wa Algeria

Naye beki Anele Ngcongca anaamini kwamba licha ya upande wao kutokuwa na wachezaji wenye majina makubwa kutoka ligi za ulaya wana uwezo wa kushindana.

"Kujiamini na morali ya timu iko juu sana,tunataka kwenda huko na kuwahakikishia kuwa Afrika Kusini kuna vipaji.

"Naamini tunaweza kushindana dhidi ya Algeria.Sisi sote tunafahamu ni mchezo muhimu kwa timu zote mbili na sote tunataka kuanza vizuri mashindano

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Marehemu Senzo Meyiwa

"Kikosi tulichonacho kwa sasa kiko moto na kina nguvu za ajabu , tunaangalia mbele kwenye michuano hii na ninafikiri tunaweza kuzishangaza timu nyingi.