Mafuriko yawaua watu 200 Malawi

Haki miliki ya picha
Image caption Watu 200 waaga dunia kutokana na mafuriko Malawi

Utawala nchini Malawi unasema kuwa umewaokoa maelfu ya watu ambao walikuwa wamekwama kutokana na mafuriko ambayo yameikumba nchi hiyo.

Wanajeshi walitumia mashua na ndege za helikopta kuwahamisha watu kwenda maeneo yaliyoinuka kufuatia kuharibiwa kwa barabara na madaraja.

Takriban watu 200 wameripotiwa kuaga dunia huku wengine 200,000 wakilazimika kuhama makwao.

Serikali ya msumbiji imeomba msaada wa kimataifa ambapo pia imeweka kambi ikiwa inawapa waathira chakula maji na makao.