BBC yazindua tuzo kumuenzi Komla Dumor

Image caption Aliyekuwa mtangazaji wa BBC Komla Dumor

Shirika la habari la BBC linazindua tuzo kwa heshima ya aliyekuwa mtangazaji wake Komla Dumor, mwaka mmoja baada ya kifo chake akiwa na umri wa miaka 41.

Komla Dumor alikuwa mwandishi na mtangazaji mwenye kipaji cha kipekee kutoka nchini Ghana huku akisifika sio Ghana pekee bali Afrika na duniani kote.

Aliwakilisha Afrika kama bara lenye kujiamini na lenye wajasiri amali wengi.

Kupitia kwa kazi yake ya uandishi na kusimulia taarifa kwa wengi, Komla alifanya kazi kwa kujitolea sana kutoa taswira tofauti kuhusu Afrika kwa dunia nzima.

Shirika la BBC limejitolea kuandeleza kazi ya Komla.

Tunajivunia sana kama BBC kutangaza tuzo ya uandishi wa habari kwa heshima ya aliyekuwa mwandishi mahiri wa BBC Komla Dumor

Tuzo hio itakuwa inatolewa kwa wandishi wenye kipaji wanaoishi barani Afrika na kufanya kazi barani humo. Sharti ni kwamba watakuwa wana kipaji cha hali ya juu kusimulia taarifa kuhusu bara la Afrika na pia wawe wanalenga kuwa mahiri katika siku za usoni.

Kupitia kwa tuzo hio,BBC itaweza kumleta mshindi katika shirika hilo kupata ujuzi wa kazi na kusimulia taarifa kuhusu Afrika kwa dunia nzima kwa kipindi cha miezi mitatu mjini London.

Mshindi pia atapata fursa ya kutangaza kwenye televishini , redio na kuandika taarifa ambazo zitachapishwa kwenye mtandao kwa mashabiki milioni 265 wa BBC kote duniani.

Fahamu zaidi kuhusu tuzi hii ujue kama unaweza kushiriki