Waasi wapambana na wanajeshi Yemen

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waasi waliopambana na wanajeshi wa Yemen

Serikali ya Yemen imeafikia makubaliano na kundi la waasi wa Houthi baada ya masaa kadha ya mapigano makali kwenye ikulu ya rais.

Milipuko mikubwa imekuwa ikisikika mjini Sanaa na raia wengi wanaripotia kukimbia.

Lakini afisa mmoja wa kundi la Houthi anasema kuwa mapigano yamesitishwa huku rais Abed Rabbo Mansour Hadi akitarajiwa kukutana na waakilishi wa waasi hao baadaye leo.

Lacha ya mapigano kusitishwa, waasi wangali wanapiga kambi katika maeneo wanayoyadhibitihasa katika eneola Kaskazini na Kati ambako watu wa madhdbu ya Sunni wako kwa wingi.

Mapigano hayo yanajiri siku mbili baada ya waasi wa Houthi kumteka nyara mkuu wa ofisi ya rais.

Kituo cha televisheni cha waais hao, kiliripoti kuwepo makabiliano makali baada ya wanjeshi kuwafyatulia risasi wanajeshi wanaopambana na uasi.

Afisaa mmoja wa jeshi alisema kuwa waasi hgao ndio walioanza mashambulizi.

Waasi wamekuwa wakipiga kambi katika mji wa Sanaa baada ya kufanya vurugu mwezi Septemba mwaka jana.