Wanafunzi wapinga unyakuzi wa ardhi Kenya

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Polisi waliwafyatulia wanafunzi gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya

Polisi nchinikenya katiika mji mkuu Nairobi leo imewafyetulia gesi ya kutoa machozi wanafunzi wa shule ya msingi waliokuwa wakiandamana kupinga unyakuzi wa ardhi waliyokuwa wanatumia kama kiwanja cha kuchezea na mmiliki binafsi.

Polisi hao wakiwa na Mbwa waliwatawanyta wanafunzi hao, baadhi yao wakisemekana kuwa watoto wenye umri wa miaka sita baada ya kuuangusha ukuta mpya uliojengwa kati ya shule yao na uwanja huo.

Wanafunzi hao walikuwa wamerejea shuleni Lang'ata baada ya mgomo wa wiki mbili wa walimu wa shule za umma walipopata kiwanja chao kikiwa kimeuzwa na hata kuwekwa uzio.

Shule hio ina karibu watoto 1,000 walo kati ya umri wa miaka mitatu na kumi na minne na inasimamiwa na baraza la jiji.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wanafunzi hao walikuwa wamerejea shuleni baada ya mgomo wa wiki mbili wa walimu wa shule za umma

Wanafunzi kadhaa walijeruhiwa katika purukushani hilo wakati polisi walipoingilia kati na kujaribu kuwatawanya wanafunzi hao waliokuwa wanazua rabsha.

Baadhi yao walipelekewa hospitalini baada ya kupata majeraha madogomadogo.

Baadhi ya wanafunzi hao walikabiliana na polisi wakiwa wamebeba vijiti na kuwanyoshea.

Polisi mmoja alijeruhiwa baada ya kupigwa kwa mawe.

Walimu wa shule hio pia waliandamana wakisaidiwa na wanaharakati wa kisiasa.

Haijajulikana ambavyo mtu huyo aliweka uzio katika kiwanja hicho walichokuwa wakitumia wanafunzi kuchezea.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wanafunzi wakigonga uzio uliokuwa umewekwa katika ardhi hio iliyonyakuliwa na mtu asiyejulikana

Baraza la jiji limesema kuwa ardhi hio ni ardhi ya serikali ingawa halijazungumzia ambavyo ardhi yenyewe iliuzwa ingawa wanaharakati wanasema kiwanja hicho kimeuzwa kwa tajiri anayepanga kukitumia kwa ujenzi.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Polisi mmoja alijeruhiwa katika purukushani hizo
Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Baadhi ya wanafunzi walibeba vijiti na kuwafukuza polisi