Afariki akicheza mchezo wa video

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Vijana wanaocheza michezo ya video

Mtu moja mwenye umri wa miaka 32 huko Taiwan amefariki baada ya kucheza michezo ya mitandaoni,ikiwa ni kisa cha pili kwa mchezaji kama huyo kuaga dunia.

Imebainika kuwa mtu huyo aliaga dunia masaa kadhaa huku wenzake wakiendelea kucheza bila kujua.

Alipatikana amelala katika meza moja ndani ya mgahawa wa mitandao mnamo Januari 8 akiwa hana uhai na kulazimika kupelekwa hospitalini ambapo alitangazwa kwamba amefariki.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Vijana wakicheza michezo ya mitandaoni

Mtu huyo kwa jina Hsieh alikuwa akicheza mchezo huo katika mgahawa wa Kaohsiung,ambao ndio mji wa pili kwa ukubwa nchini Taiwan tangu january 6.

Mtu huyo ambaye hakuwa na ajira alipendelea sana kutembelea migahawa ya mitandao polisi walisema.Inadaiwa kwamba mtu huyo angetoweka kwa siku mbili ama hata tatu kwa mara moja.

Maafisa wa Polisi wamesema kwamba wachezaji wa mchezo wa mtandao katika mgahawa huo waliendelea kucheza bila kugundua ni nini haswa kilichotokea licha ya maafisa hao pamoja na madktari kuwasili ili kumchunguza mtu huyo.