Viongozi Afrika na mvutano wa Madaraka

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Robert Mugabe

Kama sehemu ya Siku ya Demokrasia ya BBC, Maulid Julien anawatazama Viongozi wa Afrika waliokataa kuondoka madarakani na wale walioondolewa kwa mabavu na Raia au waandamanaji.

Maana nzima ya demokrasia kuwa Serikali iliyochaguliwa na Watu kwa ajili ya Watu imekuwa haitiliwi maanani na Viongozi wa Afrika ambao hawataki kuondoka madarakani.

Mifano ya wazi kabisa ya ni pamoja na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe na Rais wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang Nguema.

Viongozi wengine kadhaa ni Rais wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila na wa Burundi Pierre Nkurunziza ambao wameonesha nia ya kuendelea kuongoza nchi zao.

Wakati huohuo, nchi kadhaa, zikiwemo Senegal na Burkina Faso, zimeshuhudia maandamano miaka ya karibuni, yakishinikiza Viongozi wake kuondoka madarakani.

Hatua hiyo imeleta matumaini kuwa marais wengine hawatang'ang'ania kubaki madarakani baada ya muda wao kama unavyoonyeshwa kwenye Katiba kuisha.

Burkina Faso:

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Burkina Faso Blaise Compaore

Rais Blaise Compaore, 63, ameongoza kwa miaka 27.alinyesha nia ya kubadili katiba Mwezi Oktoba mwaka 2014 ili kuwania tena mwezi Novemba mwaka 2015.

Wabunge walijadili mswada wa mabadiliko ya katiba,maelfu ya Watu walivamia Bunge, Makao makuu ya chama tawala na Ikulu.Rais alijiuzulu baada ya siku nne za maandamano, na Serikali ya mpito ikaundwa.

Senegal:

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa zamani wa Senegal Abdoulaye Wade

Aliyekuwa Kiongozi wa nchi hiyo, Abdoulaye Wade aliongoza kwa awamu tatu ingawa Katiba ya nchi hiyo inakataza kutawala kwa zaidi ya awamu mbili.

Mahakama ya katiba iliamua kuwa kwa kuwa Katiba iliandikwa baada ya kumalizika kwa awamu yake ya kwanza, anaweza kuwania tena uchaguzi wa mwaka 2012.

Lakini tangazo hilo lilisababisha maandamano ambayo yaliendelea mpaka siku ya uchaguzi.Rais Wade hatimaye alikubali kushindwa baada ya kura na mshindani wake Macky Sall.

Burundi:

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza

mwaka 2015 itaelekea kwenye uchaguzi, uchaguzi ambao unaonekana kuwa na msuguano.Pierre Nkurunziza alikuwa Rais wa kuchaguliwa wa Burundi baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2005.

Miaka kumi baadae , Vyama vya upinzani vinasema Rais anatishia kukiuka sheria iliyomuweka madarakani.

Katiba ya Burundi inaeleza Rais atatumikia kwa awamu mbili pekee,lakini yeye amekuwa madarakani kwa kupindi cha miaka 10, Watu wanaomuunga mkono wanasema miaka mitano ya kwanza haihesabiki kwa sababu alichaguliwa na bunge la nchi hiyo na sio kura ya Raia wote.

Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo:

Haki miliki ya picha
Image caption Rais wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila

Rais Joseph Kabila amekuwa madarakani tangu Baba yake Laurent alipouawa mwaka 2001.

Anatawala kwa muhula wa pili, na Katiba ya nchi hiyo haimruhusu kuwania urais kwa awamu ya tatu katika uchaguzi wa mwaka 2016.

Lakini msemaji wa Serikali Lambert Mende amesema kuwa zoezi la upigaji kura linaweza kuchelewa kwa sababu ya zoezi la kuhesabu watu nchi nzima ambalo huenda likaanza mwaka huu na kuchukua miaka mitatu.

Upinzani hauungi mkono mswada wa Sensa, wakidai kuwa hizo ni njama za kumfanya Rais aendelee kuwa madarakani.

Guinea ya Ikweta:Rais aliyekaa madarakani muda mrefu zaidi kuliko wote baranai Afrika,Teodoro Obiang Nguema, 72 Mwanajeshi wa zamani amekuwa akiongoza nchi hiyo kwa miaka 36.

Aliingia madarakani mwaka 1979 baada ya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Mjomba wake Francisco Macias Nguema, ambaye baadae aliuawa.

Haifahamiki kama atawania tena urais,hajaonesha nia yoyote pia ya kutowania urais.Mtoto wake,Teodorin Nguema Obiang,ni Makamu wa pili Rais wa nchi hiyo ambaye anaelezwa kuwa pengine atarithi wadhifa huo.

Zimbabwe:

Haki miliki ya picha no
Image caption Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na mkewe Grace Mugabe

Robert Mugabe ni Rais mwenye umri mkubwa barani Afrika, ameiongoza Zimbabwe kwa miaka 34.ana miaka 90,anakaribia mwisho wa utawala wake, lakini mkewe Grace anaonekana kuja kumrithi Mugabe.

Hivi karibuni alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Zanu-PF tawi la Wanawake.

Grace alikuwa katika Kampeni za kumuondoa madarakani aliyekuwa Makamu wa Rais Joyce Mujuru ambaye alikisiwa kumrithi Mugabe.

Katiba mpya ya Zimbabwe mwaka 2013 iliweka ukomo wa miaka mitano kwa muhula mmoja kuongoza nchi, hata hivyo sheria hiyo haitekelezwi na Mugabe.