The Sun kutoshapisha picha za utupu

Haki miliki ya picha PA
Image caption Jarida la The Sun lia mazoea ya kuchapisha picha za wanawake wakiwa kifua wazi

Gazeti la The Sun limesimamisha uchapishaji wa picha za wanawake walio nusu uchi katika ukurasa wa tatu, wa gazeti hilo. Hii ni kwa mujibu wa gazeti la The Times.

The Times, ambalo lina mchapishaji sawa na gazeti la The Sun, linasema kuwa toleo la ijumaa ndilo litakuwa la mwisho kuchapisha wanawake walio nusu uchi, lakini wataendelea kuchapisha katika mtandao.

Ukurasa wa tatu umekuwa wa kuchapisha vipengele kwa miaka 44 lakini umekosolewa kwa kukiuka sera za jinsia na umepitwa na wakati.

Waandishi wa habari waThe Sun hawadhibitishi wala kukataa ripoti hii.

'Mwelekeo wa Haki’

Gazeti la The Sun lilikuwa tayari limesitisha uchapishaji wa picha zilizo nusu uchi katika toleo la mwisho wa wiki, na wakati mwingine walifanya hivyo katikati mwa wiki.

Ukurasa wa Tatu wa The Sun ulichapisha picha za mwanamitindo Rosie Huntington-Whiteley akiwa amevalia nguo za ndani pekee mnamo Jumatatu na waigizaji wa Hollyoaks Jennifer Metcalfe na Gemma Merna wakiwa wamevalia bikini ufuoni siku ya Jumanne.

The Times, gazeti ambalo linavuma Uingereza, linasema kuwa gazeti la The Sun liliamua kisitisha uchapishaji wa kipengele hicho bila ya kujulisha kila mtu. Inaripotiwa kuwa mwenye kiti mtendaji wa News Corps Rupert Murdoch ametia saini uamuzi wa kusitisha uchapishaji wa kurasa hizo.

Picha za wanawake walio nusu uchi zimepelekea kuwepo na maandamo kutoka kwa wanaharakati , huku zikivutia dua katika mtandao wa internet kufikisha saini 215,000.

Kikundi cha wanaharakati kinachojiita ‘No More page three’ Kilianzishwa mwaka 2012 na Lucy-Anne Holmes, na tangu wakati huo kimeumgwa mkono na wabunge kadhaa wanaopinga vitendo vya ngono.

Bi Holmes aliiambia BBC, kundi hilo halitadai ushindi iwapo wanawake waliovalia nguo zisizositiri mwili inavyotakina wataendelea kuchapishwa magazetini, lakini kudai ushindi huo itakuwa hatua mwafaka iwapo hawatavalia hivo.

Alisema: "The Sun hawajaamua ghafla kuwa wanawake wanafaa kusema, kufikiri, na kutenda mambo ya kuvutia, bali kimsingi wanasema kuwa wanawake wapo kwa ajili ya mapambo. "