Utata kuhusu idadi ya waliouawa DRC

Image caption Vurugu mjini Kinshasa zimechochewa na mswada tatanishi kuhusu uchaguzi

Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRC ,Lambert Mende ameambia BBC kwamba takriban watu 11 wakiwemo raia wameuawa mjini Kinshasa tangu vurugu zilizosababishwa na mswada tatanishi wa uchaguzi kuanza Jumatatu.

Mswada huo umetajwa na wanasiasa wa upinzani kama mapinduzi ya kikatiba wakisema utamfanya Kabila kujiongeza muda mamlakani kwa miaka mingine mitatu.

Mswada huo unajadiliwa na baraza la senate huku viongozi w aupinzani wakiitisha maandamano mengine hii leo kuupinga mswada huo.

Haki miliki ya picha
Image caption Serikali inasema watu 11 wameuawa tangu Jumatatu wakati upinzani ikisema idadi kamili ni 28

Bwana Mende alisema kuwa wale waliouawa walikuwa wananchi 10 waliouawa na walinzi wakati walipokuwa wanapora maduka ya watu binafsi huku polisi mmoja akipigwa risasai na melnga shabaha.

Alisema watui wengine 22 walijeruhiwa wengi wao wakiwa polisi.

Aliongeza kwamba wengi wa waandamanaji walikuwa wamejihami kwa silaha miongoni mwao wakiwa wanajeshi. Alisema watu 321 walikamatwa kwa kuharibu mali ya watu binafsi au ya umma na kwamba watafikishwa mahakamani leo.

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Kabila anadaiwa kupanga njama ya kutaka kujiongeza muda zaidi mamlakani

Alikanusha madai kuwa polisi walitumia silahakali dhidi ya waandamanji akisema kwamba walitumia tu gesi ya kutoa machozi na virungu.

Baraza la Senate linatarajiwa kudadadisi mswada huo tatanishi ambao ulichochea maandamano hayo huku viongozi wa upinzani wakiitisha maandamano zaidi ingawa wamelaani visa vya uporaji.

Kiongozi wa upinzani Vital Kamerhe aliambia BBC kwamba waandamanaji 28 waliuawa kuanzia Jumatatu kinyume na idadi iliyotolewa na serikali.

Shule za umma zimefungwa hadi Jumatatu wiki ijayo.