Msaidizi wa Mandela azua ubaguzi

Image caption Nelson Mandela na msaidizi wake wa kibinafsi Zelda le Grange

Miaka 20 ya kuwa msaidizi wa Nelson Mandela na kuwa mfano mwema maridhiano ya rangi baada ya miaka mingi ya ubaguzi nchini Afrika Kusini imefutwa katika ujumbe wa mtandao wa Twitter.

Hicho ndio kisa kilichompata Zelda La Grange msaidizi binafsi wa Nelson mandela aliyechaguliwa na shujaa huyo kumsaidia kwa kuwa familia yake ina mizizi ya jamii ya Afrikaaner.

Jamii ya Afrikaaner ilionekana kama ndio iliokuwa ikisukumu gurudumu la mfumo wa ubaguzi wa rangi.

Ni sababu hii ilioimfanya rais Mandela kusisitiza kupata msaidizi wake wa kibinasfi kutoka jamii hiyo licha ya kufungwa miaka 27 jela ili kuionyesha dunia kwamba alipendelea sana kuwaunganisha weupe na weusi nchini Afrika kusini.

Lakini iliwashangaza wengi baada ya ujumbe ulioandikwa katika mtandao wa twitter kutoka kwa msaidizi huyo wa kibinafsi wa marehemu Mandela kuonyesha kwamba alikuwa akipuuza madhara ya ubaguzi wa rangi na ukoloni miongoni wa raia wengi wa Afrika kusini.

Hivi ndivyo ujumbe huo ulivyosema.''Iwapo ningekuwa mwekezaji mweupe ningeondoka taifa hili.Ni wazi kutoka kwa rais Zuma kwamba watu weupe hawatakikani Afrika ya kusini'',.

Ujumbe huo ulizua hisia kali miongoni mwa raia huku baadhi ya wachanguzi weusi wa maswala ya kijamii wakisema kuwa sio kodi ya wazungu pekee inayojenga Afrika ya kusini.