Haki elimu yakosoa BRN Tanzania

Nchini Tanzania mpango wa maendeleo ulioanzishwa na serikali ya nchi hiyo kwa ajili ya kuleta matokeo ya haraka, unaoujulikana matokeo makubwa sasa umekosolewa na taasisi ya kiraia ya Haki Elimu kwamba haujafanikiwa katika sekta ya elimu.

Awali Jopo la Kimataifa lililotathimini mpango huo katika taarifa yake lilionyesha mpango huo umekuwa na mafanikio katika sekta zilizopewa kipau mbele ambazo ni miundo mbinu, kilimo, maji , elimu Nishati, fedha na usafirishaji.

Mwaka 2013 mpango wa mafanikio makubwa sasa ikiwa ni sehemu ya jitihada za serikali ya Tanzania kuinua uchumi kutoka uchumi wa chini hadi uchumi wa kati hadi kufikia mwaka 2025.

Katika nchi za Afrika,mpango huu umeshaleta mafanikio makubwa kwa nchi kama za Nigeria na Rwanda,hivi karibuni jopo la kimataifa za tathmini likiongozwa na raisi wa zamani wa Ghana Festus Moghae alisema mpango huo unafanikiwa pia katika nchi ya Tanzania.

Ingawa mpango huo umekosolewa katika baadhi ya maeneo ikiwemo suala la Elimu,kuwa malengo yake bado hayajafikiwa ukilinganishwa na dira ya mpango huo.