Watoto wa Hosni Mubarak kuachiliwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak na wanawe Alaa na Gamal wakiwa kizimbani

Mahakama nchini Misri imeamrisha kuachiliwa kwa watoto wa kiume wa rais wa zamani Hosni mubarak wakati wanaposubiri kesi yao pamoja na baba yao inayohusu ufisadi.

Wakili wa Alaa na Gamal Mubarak anasema kwa anatarajia wawili hao kuachiliwa leo.

Hasira kutokana na kile kilichoonekana kama jitihada za kumuandaa Gamal Mubarak kuweza kumrithi babake kama rais ni moja ya sababu zilizosababisha maandamano makubwa yaliyomundoa madarakani rais Hosni Mubarak.