Aomba uchaguzi ucheleweshwe Nigeria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kampeni za uchaguzi nchini Nigeria

Mshauri wa masuala ya usalama nchini Nigeria amesema kuwa ameiambia tume ya uchaguzi nchini humo kuchelewesha uchaguzi wa mwezi ujao ili wapate muda wa kusambaza kadi za kupigia kura.

Akiongea mjini London Sambo Dasukime alisema kuwa kadi milioni 30 bado zinasalia kusambazwa kote nchini Nigeria

Amesema kuwa ni kadi milioni 39 ambazo zilisambazwa mwaka mmoja uliopita

Rais Goodlack Jonathan anawania tena urais akikabiliwa na upinzani kutoka kwa kiongozi wa zamani wa kijeshi Mohamadu Buhari.