Ujumbe wa Uturuki Somalia washambuliwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Hoteli ilioshambuliwa

Kumekuwa na shambulizi la mlipuaji wa kujitolea muhanga katika hoteli moja mjini Mogadishu nchini Somali ambapo maafisa wa Uturuki walikuwa wakijiandaa kumlaki rais Recep Teyyip Erdogan.

Takriban raia watatu wa Somali waliuawa wawili kati yao wakiwa maafisa wa usalama wakati gari lililojaa vilipuzi lilipogonga lango la hoteli.

Uturuki hatahivyo imesema kuwa hakuna mjumbe wake aliyejeruhiwa na kwamba ziara ya rais Erdogan itaendelea kama ilivyopangwa siku ya ijumaa.

Kundi la wapiganaji wa Alshabaa limesema kuwa lilitekeleza shambulizi hilo.