Matumaini mapya baada ya kupoteza Viungo

Image caption Alex Lewis amelazimika kuzoea maisha ya ulemavu

Ndani ya wiki chache Alex Lewis alitoka kuwa mmiliki wa mgahawa,na kuwa mgonjwa sana akiwa amepoteza miguu na mikono yake, hata hivyo anaeleza kuwa mwaka uliopita ni mwaka mzuri zaidi.

Mbali na kupoteza miguu yake,Lewis pia hana mdomo na amepoteza pua yake pia, wapasuaji walitumia ngozi kutoka kwenye bega lake na kutumia kuutibu mdomo wake.

Lewis anasema sasa anajiona mtu mwenye furaha kuliko alipoanza kuugua.Watu wengi hawaamini, lakini anasema mambo ameshuhudia mambo mazuri kutokana na hali yake

Image caption Mdomo wa Alex ukiwa umeharibika vibaya

Pamoja na kuwa na changamoto hizo Lewis anatimiza majukumu yake kama Baba, Mwenza,kama binaadam, ameanzisha nyumba ya kusaidia wasiojiweza ikiwa na jina lake ambapo huwasaidia wengine.ingawa amekuwa na mtazamo chanya kuhusu hali aliyonayo, hawezi kufanya kazi nyingi alizopenda kufanya awali, kama kupika na kucheza Golf.yeye na mwenza wake Lucy hivi sasa hawana mgahawa waliokuwa wakiuendesha awali.

Matumaini hafifu ya kuishi

ilikuwa Mwezi Novemba mwaka 2013 wakati Lewis alipohisi ana mafua, lakini alipogundua damu kwenye haja ndogo, kisha ngozi yake ikiwa na madoa na alama, akajua kuna tatizo kubwa mwilini mwake.

Ikabainika alipata maambukizi ambayo yalisambaa kwenye tishu zake na viungo vyake na kusababisha sumu kuingia kwenye damu yake,ilikuwa hali ya kuogopesha,viungo vya mwili wake vilishindwa kufanya kazi.

Ngozi yake ya mikono na miguu, na sehemu ya uso wake haraka ikabadilika rangi na kuwa nyeusi ikaharibika.hali hii iliwashtua sana wanafamilia na marafiki kwani hali yake ilikuwa mbaya akipumua kwa msaada wa mashine.

Miguu ya Lewis ilianza kuathiri mwili wake mara tu baada ya kutoka kwenye mashine,aliambiwa sharti akatwe mkono wake sehemu ya kiwiko.

Image caption Alex Lewis akiwa na Familia yake

Lewis anasema hakujisikia huzuni wala hisia mbaya baada ya kupatiwa taarifa hizo kwa sababu madaktari walikuwa wakimwambia hali halisi ''niliona mkono huu ndio uliokuwa ukinisababishia kuzorotesha afya yangu nikaona ni sawa ukikatwa'' alieleza.

Ilikuwa wiki ya pili ya mwezi Desemba, ingawa alipoteza mkon, hakutoka kwenye hatari ile moja kwa moja, miguu yake iliyoharibika iliendelea kusambaza sumu mwilini na kwa haraka, alilazimika kukatwa Mguu mmoja kisha wa pili, akambaki na mkono mmoja wa kulia.

Mkono wa kulia ulikuwa umeharibika pia, lakini madaktari waliona kuwa kuna uwezekano wa kuuponya.

Lakini ubovu wa mkono uliendelea kuwa mkubwa zaidi, siku moja usiku wakati alipokuwa amelala, Lewis alijigeuza na kuuvunja mkono wake sehemu mbili.

''Mkino wangu ulining'inia kwenye sehemu ya kiwiko'' anasema.Mwenza wake Lucy alishikwa na hofu akifikiria ugumu wa maisha yatakayomkabili mwenza wake wakati huu akiwa hana mikono wala miguu, Lewis anasema hakujali.

Image caption Alex Lewis akitumia viungo vya bandia

''haina maana kukaa kwa miaka mitano kwa ajili ya kuhangaika kuuponya mkono'' anasema.''nafikiri kisaikolojia ingeniathiri kusubiri kwa muda wote huo kisha kuupoteza mkono''.

Akiwa hana miguu na mikono Lewis analazimika kujifunza maisha mapya.hawezi kuamka mwenyewe, kujisafisha na kuvaa asubuhi, alilazimika kumzoea mtu anayemtunza mbaye hufika mara moja kwa siku, lakini jambo la kwanza alilokuwa akijitahidi kufanya ni kuhakikisha anajifunza kutembea akitumia viungo vya bandia.

Amekua akitembelea miguu ya bandia kwa takriban miezi mitatu na kusema kuwa anaendelea vizuri ingawa anaona kitu chaajabu kidogo.''kupanda ngazi ni ngumu kwa kuwa viungo hivi vya bandia ni vifupi''

Lewis anasema anaona bado yuko ndotoni akishangaa na kutafakari namnaambavyo mwili uliouzoea kwa miaka 33 unaweza kubadilika bila kugundua.