Aliyekua mkuu wa polisi A.Kusini afariki

Image caption Selebi amefariki akiwa na umri wa miaka 64

Afisaa wa zamani wa polisi mwenye utata nchini Afrika Kusini, Jackie Selebi amefariki akiwa na umri wa miaka 64.

Mnamo mwaka 2010 bwana Selebi alifungwa jela miaka 15 kwa kuchukua hongo kutoka kwa mlanguzi wa dawa za kulevya.

Lakini aliachiliwa kwa sababu za kiafya baada ya kifungo cha chini ya mwaka mmoja jela.

Jackie Selebi alikuwa mmoja wa maafisa wakuu wa chama tawala cha ANC kufungwa jela kwa kosa la rushwa.

Watu walilezea gadhabu baada ya kuachiliwa kwake wakisema kwamba chama kilikuwa kinamlindaili asiadhibiwe.

Bwana Selebi pia aliwahi kuwa mkuu wa shirika la polisi wa kimataifa la Interpol.