kijakazi akiri kumnyanyasa mtoto Kenya

Haki miliki ya picha Daily Monitor
Image caption Kijakazi wa Uganda alliyeshtakiwa kwa kumpiga mtoto mdogo

Msaidizi wa nyumbani mwenye umri wa miaka 18 katika mtaa wa Zimmerman, jijini Nairobi anakabiliwa na mashtaka baada ya kukiri kumlazimisha mvulana wa miaka mitatu kuramba sehemu zake nyeti.

Kwa mujibu wa jarida la The Nairobian nchini Kenya, mamaake mtoto huyo anasema kuwa mwanawe alionekana kuchanganyikiwa kila mara alipotoka kazini swala lililomlazimu kufanya uchunguzi.

Alipomuuliza mwanawe,alisema kwamba msaidizi huyo wa nyumbani alikuwa akimnyanyasa kijinsia.

Inadaiwa kuwa msichana huyo alikuwa akimlazimisha mvulana huyo kumramba sehemu zake za siri wakati mama yake anapoondoka.

Mfanyikazi huyo wa miaka 18 alikiri kufanya kitendo hicho kwa kuwa hakupewa mda wa mapumziko lakini akaomba kusamehewa.

Kwa sasa anakabiliwa na mashtaka ya kunajisi na amewachiliwa kwa dhamana ya shilingi millioni moja.Kisa hicho kinajiri baada ya kijakazi mwengine nchini Uganda kufungwa jela baada ya kupatikana katika kanda ya video akimnyanyasa kwa kumpiga mtoto mdogo.