Mfalme Abdullah:Viongozi waelekea Saudia

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kifo cha mflame wa saudia Abdullah

Viongozi kutoka sehemu mbali mbali za dunia wanasafiri kuelekea nchini Saudi Arabia kufuata kifo cha mfalme Abdullah.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron na rais wa Ufaransa Francois Hollande wanatarajiwa kukutana na uongozi mpya wa mfalme Salman kwenye mji mkuu Riyadh.

Makamu wa rais wa marekani Joe Biden ataongoza ujumbe kutoka Marekani huku Iran ikiwakilishwa na waziri wake wa mambo ya kigeni Mohammad Javad Zarif.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri mkuu wa Uingereza david cameron na rais wa Ufaransa Francois Hollande kuelekea Saudia kufuatia kifo cha mfalme Abdullah

Mfalme Abdullah ambaye alikuwa na miaka 90 alizikwa kwenye kaburi lisilotambuliwa siku ya Ijumaa.

Mrithi wake ambaye ni nduguye wa kambo Salman anasema ataendeleza sera zake.