MSF:Sudan ilishambulia hospitali

Haki miliki ya picha
Image caption Jeshi la Omar el Bashir ladaiwa kushambulia hospitali kusini mwa Kordofan

Shirika la madaktari wasio na mipaka Medecine Sans Frontieres limeilaumu Sudan kwa kushambulia moja ya hospitali katika jimbo la Kordofan Kusini ambapo wanajeshi wa serikali wanapigana na waasi.

Shirila hilo linasema kuwa jeshi la wanahewa la Sudan lilidondosha mabomu 13 ndani na nje ya hospitali hiyo kwenye milima ya Nuban ambapo watu wawili walijeruhiwa.

Serikali ya Sudan awali imekana kuwalenga raia katika kampeni yake dhidi ya waasi katika jimbo la kordofan Kusini.