Waziri atekwa nyara na wanamgambo Libya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption mashambulizi libya

Wanamgambo wamemteka naibu waziri wa maswala ya kigeni katika serikali inayotambuliwa kimataifa.

Maafisa wanasema kuwa Hassan al Saghir alitekwa nyara kutoka chumba chake cha hoteli katika mji wa mashariki wa Al-Baida mapema jumapili.

Haijulikani ni kundi gani lililotekeleza kisa hicho.

Utekaji nyara umekuwa jambo la kawaida nchini Libya,ambapo serikali mbili zinapigania udhibiti huku makundi tofauti ya wanamgambo yakikabiliana.