Jeshi lakabiliana na Boko Haram Nigeria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa Nigeria wawasaka wapiganaji wa Boko Haram

Jeshi la Nigeria linasema kuwa linapambana na shambulizi linalokisiwa kuwa la Boko Haram kwenye mji ulio kaskazini mashariki wa Maiduguri . Wenyeji wanasema kuwa walisikia milipuko mikubwa.

Barabara zote zimefungwa na eneo hilo limezingirwa.

Jeshi linasema kuwa linawashambulia wanamgambo hao ardhini na angani

Rais Goodluck Jonathan aliutembelae mji huo jana Jumamosi katika kampeni ya uchaguzi na kuahidi kumaliza mashambulizi ya boko haram eno hilo.