Rais wa Uturuki awasili Somalia

Haki miliki ya picha DHA
Image caption Rais Erdogan akifungua miradi ya maendeleo Somali

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amewasili katika mji mkuu wa Mogadishu nchini Somalia ambapo anafungua miradi kadhaa ya ujenzi ya Uturuki.

Usalama umeimarishwa katika mji huo pamoja na ikulu ya rais huku mamia ya maafisa wa polisi pamoja na wanajeshi wakipiga doria katika kile kinachoonekana kama ziara isiyo ya kawaida ya kiongozi wa kimataifa.

Uturuki ni mwekezaji muhimu wa Somalia ambayo inaendelea kujengwa.

Siku ya Alhamisi hoteli moja iliokuwa ikiishi ujumbe wa Uturuki ilipigwa na bomu lililotegwa ndani ya gari na kundi la Alshabaab.

Mara ya mwisho kwa rais Erdogan kuzuru Somalia ni mwaka 2011 ambayo ilikuwa ziara ya kwanza kwa kiongozi kutoka nje ya bara Afrika.