Lupita ang'ara katika tuzo za wasanii

Image caption lupita

Umaarufu wa msanii Lupita Nyong'o katika Red Carpet nchini Marekani haujashuka licha ya kutokuwepo katika kamera kwa miezi michache iliopita.

Mara yake ya pili katika Red Carpet ilikuwa siku ya jumapili usiku ambapo maonyesho ya tuzo la wasanii wa Filamu SAG yalifanyika,ambapo aliwaacha wengi vinywa wazi.

Akiwa amevalia rinda refu lenye rangi nyingi la mwanamitindo Ellie Saab ,msanii huyo nyota katika filamu ya 12 years slave aliwafanya waliohudhuria tuzo hizo kutaka kumuona yeye tu.

Lakini kile kilichovutia wengi ni mtindo wake wa nywele.

Akifuata mizizi yake ya Afrika ,lupita ambaye hupendelea sana kuweka nywele fupi mara hii alizisuka nyewele hizo.

Image caption Lupita Nyongo

Tuzo hiyo inajiri baada ya onyesho lake la kwanza katika Red carpet ambapo alivalia vazi la Giambattista.

Vazi hilo lililokuwa na rangi za zambarau na nyeupe lilizua hisia tofauti miongoni mwa mashabiki na wapendwa wa fesheni.

Hathivyo rinda lake katika tuzo ya SAG liliwavutia wengi na huku mtindo wake wa nywele ukiwa wa kurembesha zaidi.